Tangazo

November 27, 2015

MAKUNDI YA JAMII ASILIA YA WAHADZABE, WABARABAIG, WAMASAI WAIOMBA SERIKALI YA TANZANIA KUWATAMBUA KAMA JAMII NYINGINE

DSC_0928
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mh. Idd Ramadhan Mapuri (katikati) akizindua taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania. kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay na (kulia) ni mmoja wa wajumbe walioshiriki kuandaa ripoti hiyo, kutoka nchini Kenya katika taasisi ya ACHPR, Dk. Naomi Kipuri.(Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Na Andrew Chale, Modewjiblog

[DAR ES SALAAM-TANZANIA] Jamii ya watu wa asili na makundi yao wameiomba Serikali ya Tanzania kutambua uwepo wao hapa nchini ikiwemo kuwatangaza kwa mema na kuwasaidia kwa misingi ya haki, hutu na kimaendeleo kama watu wengine wanaotambulika ndani na nje ya mipaka yao.

Hayo yameelezwa mapema leo jijini hapa wakati wa uzinduzi wa taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania wakiwemo makabila ya Wa-Akiye,Wa- Hadzabe,Wa- IIparakuyio Masai na wengine wengi.

Akielezea katika uzinduzi huo mmoja wa wajumbe walioandaa taarifa ya Tume hiyo, ambaye anatoka nchini Kenya, katika taasisi ya African Commission on Human and Peoples Rights (ACHPR), Dk. Naomi Kipuri amebainisha kuwa jamii ya watu asilia wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha kutaka kupata haki zao zao msingi na kutambulika zaidi.

“Utafiti tuliofanya jamii ya watu asilia wamekuwa katika malalamiko ya muda mrefu ikiwemo kutaka haki zao za msingi. Ikiwemo masuala ya elimu, makazi na haki zingine. Pia wameomba Serikali kuwatangaza watu hawa wa asilia ili wasionekane wageni kwani jamii nyingi bado hazijawatambua na hata kupelekea kuwavunjia hutu wao” alieleza Dk. Naomi.

Aidha, Dk. Naomi katika uwakilishi wake wa mada kwenye mkutano huo amelezea namna ya jamii inavyoendelea kuwaona watu hao ni tofauti kiasi cha kupelekea watu hao kudumaa na maisha yale yale ya asilia.
DSC_0961
Mtangazaji wa radio Deutsche Welle (DW) ya Ujerumani, George Njogopa akifanya mahojiano na Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay. Kushoto ni Mratibu wa NGONET Ngorongoro, Samweli Nangiria 

  “Jamii zingine zinawatenga watu wa jamii ya Wamasai, tumeshuhudia lugha na matamshi kwenye mizunguko ya watu ikiwemo kwenye madaladala, mitaani huku wakimuona Mmasai kama mtu tofauti, sasa katika ripoti hii imeweza kuelezea mambo mengi sana. 

Ikiwemo suala la Haki ya kuishi, kufanya kazi na mambo yote kama watu wengine” alimalizia Dk. Naomi. 

  Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mh. Idd Ramadhan Mapuri ameeleza kuwa kupitia ofisi yake itahakikisha inashughulikia suala hilo la kuwa karibu na watu asilia na kutambua misingi ya haki zao ambapo amebainisha watu hao wa asilia kwa Tanzania wanafikia makundi zaidi ya sita. 

  Kwa upande wao baadhi ya wawakilishi wa watu hao wa watu asilia wakielezea katika mkutano huo, waliomba na wao na wapate wawakilishi maalum ikiwemo Bungeni ama sehemu za maamuzi ikiwemo Halmashauri na maeneo mengine ya Serikali ilikutambua michakato ya Kimaendeleo kwa kina. 
  “Jambo la ardhi, ndilo linalotuumiza kwa sasa. Sie tunaporwa ardhi yetu kila siku na kesi nyingi ni za kuporwa ardhi na migogoro ya wakulima na wafugaji, ndani ya migogoro hii ina siri kubwa bila kujua kiini chake ni wakati wa kufika kule na kupata ukweli zaidi” alielezea Adam Ole Mwarabu 

  Kwa upande wake, Mratibu wa NGONET Ngorongoro, Samweli Nangiria ambaye anawakilisha watu hao asilia anaeleza kuwa, wao wamekuwa wakitambuana kwa desturi ikiwemo suala la ufugaji na maisha mengine, Jamii nyingine imekuwa wakiwaona wao ni watu wa tofauti kiasi cha kupora mali zao ikiwemo ardhi, mifugo na mambo mengine ya msingi.
DSC_0953
Baadhi ya wawakilishi wa Jamii za watu asilia wakiwemo Wahadzabe, Masai, Wabarabaig na wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na wadau wengineo wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo juu ya usawa na kutambulika kama jamii asilia yenye tamaduni na desturi zake.

“Sie watu asilia tuna mahusiano mbalimbali na jamii zetu za kifugaji licha ya jamii zingine kutuingilia kwenye maeneo yetu na kupora ardhi yetu. Watu asilia tunahitajika kutambulika zaidi na hata kupatiwa huduma muhimu ikiwemo kujengewa shule, vyuo na mahitaji mengine ikiwemo haki na hutu kama watu wengine.” Alieleza Samweli Nangiria.

Kwa upande wake, .. ameweza kuipongeza tume ya Haki za Binadamu kwa kuweza kushughulikia suala hilo na hata kuandaa tukio hilo kwa kushirikisha wadau wengine wakiemo wao wa asilia.

“Tanzania ndio nchi ya kwanza kuaandaa kikao cha Afrika kwa watu hawa wa makundi maalum wa asilia, kilichofanyika mwaka uliopita. Hili ni jambo bora sana kwani watu asilia tunaendelea kutambulika zaidi.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa ya taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania, imeweza kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo suala la haki ya kuishi, Utawala bora na namna ya jamii hizo zinapotokea katika maeneo yao hapa nchini.

DSC_0944
Wadau wa haki za binadamu wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano huo baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo ya kuwatambua watu wa makundi asilia. Mkutano unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Blue Pearl Ubungo jijini Dar es Salaam.
DSC_2541
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo Mhifadhi Mkuu, kutoka ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Seleman Kisimbo akichangia mada juu ya hali iliyopo sasa ikiwemo jamii hiyo ya watu asilia na changamoto za Mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo suala la ukame inayowakabili katika maisha yao ya vijijini.
DSC_0946
Dk. Naomi Kipuri wa taasisi ya ACHPR, ya nchini Kenya akijadiliana jambo na Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Tumaini-Makumira, Bw. Elifuraha Laltaika.
DSC_0955
Baadhi ya wawakilishi wa Jamii za watu asilia wakiwemo Wahadzabe, Masai, Wabarabaig na wengineo wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye mkutano huo.

No comments: