Tangazo

July 30, 2015

MUDA WA KUJIAJIKISHA DAR WAONGEZWA

Na Magreth Kinabo
 
Tume Taifa ya Uchaguzi(NEC) imeongeza  siku nne  zaidi   kwa mkoa  wa jiji la Dar es Salam  kujiandikisha   katika daftari la kudumu la kupiga kura   ili kuwezesha wakazi wengi  kujiandikisha.
 
 Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dares Salaam Mwenyekiti  wa  tume hiyo  Jaji Mstaafu Damian Lubuva (pichani), alisema uamuzi huo umetokana  na kuwepo kwa  mwamko mkubwa  wa wananchi waliojitokeza  kwa wingi  isivyo kawaida katika vituo mbalimbali.
 
“Tume imeamua kuongeza musa wa kulizia watu watakaokuwapo vituoni siku ya mwisho yaani kesho tarehe 31,Julai, mwaka 2015. Sasa  muda umeongezwakwa siku nne ili kumalizi unadikishaji huo,|” alisema Jaji Lubuva.
 
Jaji aliongeza kwamba   hivi  sasa hadi kufikia jana tarehe 29, Julai wananchi waliojiandikisha  katika daftari hilo ni 18,826,718 kwa nchi nzima , wakati lengo lilikuwa ni kufikia wananchi milioni 23 hadi 24.
 
Alisema hadi siku ya jana watu waliojiandikisha katika jiji hilo ni 1,754,725  sawa na asiliamia   62.4,wakati makadrio ni watu 2,810,423. 

No comments: