Tangazo

April 18, 2015

Marufuku kupiga kelele Tanzania

Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Maku wa Rais - Mazingira, Mh. Binilith Mahenge (pichani), amezindua Kanuni mpya ya Mazingira itakayodhibiti uchafuzi wa mazingira unaotokana na makelele yanayosabishwa na shughuli mbalimbali katika jamii .

Akizungumza katika uzinduzi wa Kanuni hizo  jijini Dar es Salaam, Mh. Mahenge alisema kuwa Ofisi yake ilishazitangaza Kanuni hizo katika Gazeti la Serikali tangu tarehe 30/01/2015 kulingana na Sheria ya Usimazi wa Mazingira ya mwaka 20104.

Aidha Mh. Mahenge aliongeza  kuwa Sheria hiyo ya Mazingira ya mwaka 2004 iliyoanza kutumika rasmi  tarehe 1 Julai, 2015 inaiwezesha  Ofisi yake kuandaa na kuunda kanuni mbalimbali za mazingira ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira nchini.

Hata hivyo alifafanua kuwa kanuni mpya za kudhibiti kelele, hazitadhibiti kelele zitokanazo na ving`ora vya magari ya Polisi, magari ya zimamoto, magari ya kubebea wagonjwa pamoja na  mizinga wakati wa magwaride katika sherehe za kitaifa.

Kanuni hizi zimeundwa kuitikia wito wa malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali waliokuwa wakiilalamikia serikali kuhusu uchafuzi mkubwa wa mazingira unaotokana na kelele katika kumbi za starehe, uchimbaji wa madini pamoja namitetemo inayosabishwa na minara ya simu.

No comments: