Tangazo

April 17, 2015

Mamia wamzika Che Mundugwao wakiwamo wanamuziki ‘kiduchu’


Na John Badi wa Daily Mitikasi Blog
Dar es salaam 

MAMIA ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwemo wanamuziki ‘kiduchu’ leo wameshiriki katika mazishi ya Mwanamuziki Chigwele Che Mundugwao katika makaburi ya Tegeta jijini.

Baadhi ya watu waliohudhuria mazishi hayo walionyesha kutoridhishwa na mahudhurio hayo kiduchu ya wanamuziki na kulaumu chini chini kuwa kukosekana kwa ushirikiano kati ya wasanii wa muziki nchini ndilo jambo linalopelekea tasnia kuporomoka kila kunapokucha.

Shughuli za mazishi zikiendelea. PICHA ZOTE/DAILY MITIKASI BLOG
 "Huenda mahudhurio haya kiduchu yanatokana na wengi kutopata taarifa mapema wengi wao wakifikiri huenda Marehemu Che Mundugwao angesafirishwa kwenda kuzikwa kusini” alisema mmoja wa wanamuziki wakonge hapa nchini ambaye hakutaka jina liwekwe katika mtandao huu.

Aidha Daily Mitikasi Blog iliweza kuwashuhudia wanamuziki waliohudhuria msiba na mazishi hayo,  kuwa ni pamoja Kiongozi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Luiza Mbutu, Kalola Kinasha na Ras Innocent Nganyagwa.


 Viongozi wa Taasisi mbalimbali za sanaa nchini waliohudhuria ni pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, Rais wa Muziki wa Rhumba Tanzania na mdau wa muziki nchini, Francis Kaswahili.
Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza (wa pili kushoto), Ras Inno (wa pili kulia) na wadau wakiwa mazishini.
Mmiliki na Mhariri Mkuu wa Blog hii, John Badi (kushoto) akiwa na wadau wakati wa  mazishi katika makaburu ya Tegeta. Wa (pili kushoto) ni Kaka Bonda.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

BASATA YATUMA RAMBI RAMBI 

Ikiwa ni siku moja tu baada ya kutokea kifo cha Msanii Chigwele Che Mundugwao  (48)  pichani kulia Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) wametuma salamu za rambirambi za msiba huo na kusema wamepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha msanii wa muziki wa asili Chigwele Che Mundugwao kilichotokea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam leo Asubuhi ya Alhamisi 16 Aprili mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Mkuu Godfrey Mngereza ilimwelezea  marehemu Che mundugwao  kuwa alikuwa  msanii wa muziki wa asili na mdau wa muda mrefu katika  sekta ya sanaa nchini.

Pia Che  atakumbukwa kwa kuwa na mchango mkubwa katika kukuza muziki wa asili nchini na baadaye kupitia Chama cha Muziki wa asili (TAFOMA) nchinijinsi  alivyoshiriki kikamilifu kwenye mchakato wa uanzishwaji wa Shirikisho la Muziki nchini  ambalo linaviunganisha vyama vya wasanii wanamuziki.

Mchango wake katika muziki wa asili na katika kujenga mfumo wa utawala wa wasanii nchini hautasahaulika kamwe. Ni mdau aliyeacha misingi katika sekta ya muziki na amejitolea kwa kiasi kikubwa katika kuufikisha muziki huu mahali ulipo leo.

Baraza, wasanii na wadau wote wa sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote aliyotuachia marehemu Che Mundugwao hasa katika kupenda kujitolea muda mwingi kufanikisha ufanisi kwenye sekta ya sanaa.

Baraza linatoa pole kwa ndugu wa marehemu, shirikisho la muziki, wasanii na wadau wote wa sanaa kwa msiba huu. Marehemu amezikwa jana saa kumi alasiri katika makaburi ya Tegeta.

Mkurugenzi wa bendi ya Kilimanjaro Waziri Ally alisema kwamba kwa upande wa wasanii wapepata pigo na pengo ambalo halitaweza kuzibika kwani  tangu alipomfahamu Che alikuwa ni mwanamuziki wa asili na aliyewekeza katika muziki wa asili tofauti na wasanii wengine ambao wamekuwa  wakihamahama  katika namna ya upigaji wa muziki.

‘Wengi tunaelekeza kuwa tunaelekeza hisia zetu nje kabisa ya tamaduni zetu hivyo wasanii kama Che ni wachache lakini yeye alikuwa ni moja kwa moja muziki wake ulikuwa ni wa kiasili zaidi  na ulibaki katika asili alifanikiwa kudumisha utamaduni ambao wengine walishindwa” alisema. 

Mwanmuziki huyu aliweza kung’ara hta nje ya mipaka ya nchi  hasa katika nchi za ukanda wa Scandinavia ambako alikuwa akipata mialiko mara kwa mara huku wakati mwingine akiwa anakwenda kufanya maonyesho yeye mwenyewe na wakati mwingine alikua akienda na bendi yake ya Mbega Arts iliyokuwa na maskani yake Wilaya  Bagamoyo Mkoani Pwani.

Waziri alisema kwamba kila mtu lazima ataonja mauti ila Che ametangulia hivyo wasanii waliobaki waendeleze.

Hadi mauti yanamfika alikuwa chini ya ulinzi ambako alikuwa akikabiliwa na kosa la wizi wa pasi 26 za kusafiria isivyo halali akiwa na aliyekuwa Ofisa Manunuzi wa Idara ya Uhamiaji Shemweta Kilwasha (31), Mhandisi Idara ya Zimamoto na Uokoaji Keneth Pius(37) na mfanyabiashra Ally Jabir (34). Che alikamatwa Aprili 22 2013 Yombo Makangarawe.Pia liwahi kupata tuzo kadhaa za kuziki wa sili katika tuzo za Tanzania Music Awards.  

No comments: