Tangazo

September 1, 2014

UBALOZI WA UJERUMANI TANZANIA: HATUJIHUSISHI NA MASUALA YA SIASA ZA NDANI WALA MCHAKATO WA KATIBA


Kutokana na habari za mara kwa mara katika vyombo vya habari nchini Tanzania, Ubalozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani unatamka: Serikali ya Ujerumani kimaadili haiingilii mambo ya siasa za ndani za nchi zingine.

Kutokana na hali hii, Serikali ya Ujerumani na maafisa wake hawafanyi ushawishi wowote kuhusu mwelekeo wa mjadala wa katiba unaoendelea hivi sasa nchini Tanzania.

Mashirika mengi ya Kijerumani yanafanya kazi na mawakala wa asasi za kiraia duniani kote kuimarisha shughuli za mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Aina hii ya ushirikiano hufanyika pia nchini Tanzania. Shughuli hizi hulenga hasa katika
mipango ya elimu na mafunzo. Utaratibu wa mipango hii hutolewa kwa wawakilishi wa vyama vyote vikubwa vya siasa nchini Tanzania.

Shughuli za kisiasa huwa hazisaidiwi au kufadhiliwa na mashirika haya, ambayo 
hutenda kazi zake kwa kutumia pesa zinazotolewa na Serikali ya Ujerumani.

Imetolewa na:
John Merikion,
Afisa Habari 

Email: pr-100@dare.auswaertiges-amt.de,

Tel. 022 2117409

No comments: