Tangazo

July 18, 2014

WAZIRI MAKALLA ATOLEWA CHINI YA ULINZI WA POLISI BAADA YA MKUTANO WAKE KUFANYIWA VURUGU NA CHADEMA

 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (katikati), akiongozwa polisi kuingia kwenye gari baada ya kutokea vurugu meza kuu, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Goba, Kinondoni Dar es Salaam, ambazo alidai zilipangwa kwa makusudi na viongozi wa Chadema kwa lengo la kumvulugia ziara yake ya kuwaelezea wananchi utekelezaji wa Ilani ya CCM katika suala la upatikanaji wa maji ya uhakika jijini Dar es Salaam ifikapo Septemba, mwakani. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Gari lililombeba Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, likilindwa na polisi lililopokuwa linaondoka baada mkutano wa hadhara kuvunjika kulikosababishwa na vurugu ambazo waziri alidai kuwa zilipangwa kwa makusudi na wafuasi pamoja na viongozi wa Chadema waliokuwa wakirumbana na viongozi wa CCM, katika Kata ya Goba, Kinondoni, Dar es Salaam. Makalla alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.


 Makalla akijadiliana na maofisa wa CCM na Polisi kabla ya kwenda kupanda gari na kuondoka.
 Poilisi wakiwadhibiti baadhi ya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakisababisha vurugu katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Makongo. Kinondoni.
 Polisi wakimdhibiti mmoja wa viongozi wa Chadema wakati wa mzozo uliotokea jukwaa kuu katika mkutano wa Naibu Waziri wa Maji, Makalla na wananchi wa Kata ya Goba.
 Kiongozi wa cHADEMA AKIZOZANA NA WA ccm jukwaani katika mkutano wa Makongo Juu.
 Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee akizoza jukwaani katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Goba na hatimaye kuvunjika
 Polisi wakimdhibiti mfuasi wa Chadema asiendelee kufanya fujo katika mkutano wa Waziri na Wananchi wa Kata ya Goba
 Askari wa FFU, akilinda doria wakati waziri Makalla akikagua nyumba ambazo watu wamejiunganishia isivyo halali eneo la Bonde la Msimbazi, Dar es Salaam.
 Makalla na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (kushoto) wakiangalia pampu zinazotumika kujazia maji kwenye malori yanayonyonywa kutoka kwenye mabomba ya Dawasa. Pampu hizo zilinaswa uani mwa nyumba katika eneo la Bonde la Mto Msimbazi Dar es Salam
 Waziri Makalla na viongozi wengini wakishanga kuona tanki kubwa la maji lililojengwa chini ya moja kati ya nyumba tano katika eneo hilo ambazo wamiliki wake wamejiunganishia maji ya Dawasa  isivyo halali
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia), akimhoji mchezaji wa zamani wa Simba, Dua Said ambaye alikuwa miongoni mwa watu watano waliokamatwa kwa tuhuma za kujiunganishia maji isivyo halali  kutoka kwenye mabomba ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka (Dawasa), kwenye nyumba zao zilizopo Bonde la Mto Msimbazi, Kigogo, Dar es Salaam. Makalla alikuwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maji Dar es Salaam
 Askari wakilinda doria katika eneo hilo
 Moja ya malori yanayojazwa maji katika eneo hilo. Nalo liko chini ya ulinzi
 Waziri Makalla akielezea athari zinazotokana na wizi huo wa maji ambapo alisema kuwa katika nyumba hizo tano kila siku wanaiba maji lita laki tatu, hivyo kila siku kuikoseasha serikali mapato ambapo kwa mwezi yanafikia sh. bil 1.4.
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika akielezea jinsi atakavyoshirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya ufisadi wa maji jijini na kwamba atakuwa bega kwa bega kuhakikisha mswada wa adhabu kubwa kwa wezi wa maji unapelekwa Bunge la Novemba mwaka huu.
 Mchaezaji wa zamani wa Simba, Dua Said akielezea kwa wanahabari na mbele ya Waziri Makalla, jinsi anavyoshirikiana na Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (DAWASCO), katika biashara ya kuuza maji. Dua Said alikuwa ni miongoni mwa watu watano waliokamatwa kwa tuhuma za kujiunganishia maji ya Dawasco isivyo halali katika eneo la Bonde la Msimbazi
 Bomba jipya la maji likitandazwa eneo la Makongo tayari kwa maandalizi ya kusafirisha maji kutoka Mtambo wa Ruvu Chini ambao upanuzi wake umekamilika hivi karibuni.
 Makalla akiuliza swali kwa wakandarasi kuhusu utandazaji wa bomba hilo, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Dar na Pwani.
 Waziri Makalla akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mwenyekiti wa CCM, Salum Madenge, (KUSHOTO)  Deusdedit Mtiro (kulia) walipokuwa wakimlaki alipowasili kwenye mkutano katika Kata ya Makongo.

 WAFUASI WA CHADEMA WAKISHANGILIA NA KUMTAKA WAZIRI AWAHAKIKISHIE UPATIKANAJI WA MAJI MAKONGO JUU
 Chadema na CCM wakishangilia katika mkutano huo
 Waziri Makalla akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Makongo
 Moja wa wananchi akilalamika mbele ya waziri kuhusu adha kubwa wanaipata ya maji eneo la Makongo juu
 Msafara wa viongozi wa Chadema na CCM ukielekea kwenye mkutano wa wananchi katika Kata ya Goba ambao hata hivyo ulivunjika baada ya kutokea vurugu
 WanaCCM wakimshangilia Waziri Makalla alipokuwa akihutubia wananchi katika Kata ya Makongo
 Chadema wakishangilia wakati Halima Mdee akihutubia Makongo Juu
 Mfuasi wa Chadema akilalama
 Mdee akizungumza na wanahabari baada ya mkutano wa Kata ya Goba kuvunjika
 Wana CCM WAKISEREBUKA
 MNYIKA AKIZUNGUMZA NA WAFUASI WA cHADEMA BAADA YA MKUTANO KUVUNJIKA

No comments: