Tangazo

July 30, 2014

MEMBE ASEMA DINI NDIKO KWENYE CHIMBUKO LA AMANI NA UTULIVU, ACHANGIA KITABU CHA MUFTI

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Kamilius Membe, akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, huku waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (kulia) akifuatilia mazungumzo hayo kwa pembeni, wakati wakiwa kwenye hafla ya Baraza la Idd El Fitr, leo, Julai 29, 2014, kwenye Viwanja vya Kariamjee, Jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi kwenye Baraza la Eid ElFitr, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiingia kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, akisindikizwa na  Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Kassim.
 Pinda akimsalimia Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi baada ya kuwasili ukumbini
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsalimia Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Shaaban Issa Simba baada ya kuwasili ukumbini.
 Pinda akimtazama kwa furaha wakati Mwinyi akizindua kitabu kwa furaha ambacho kimeandikwa na Sheikh Mkuu, Shaaba Issa Simba, kitabu hicho chenye jina la Al Muhtaswar ni makusanyo mbalimbali ambayo sheikh Mkuu huyo ameyakusanya na kisha kutengeneza kitambu kwa ajili ya kukisambaza nchini kote kusaidia waislam kuzingatia vyema dini hiyo. Pamoja na wadau kadhaa, Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe amechangia kuwezesha uchapishaji wa kitabu hicho.
 Mtoto  wa jijini Dar es Salaam, Arafat Msham akiduusu kitabu hicho
 Membe, Dk. Salim na Sumaye wakisoma kitabu cha Sheikh Mkuu Shaaban Issa Simba
Pinda akitoa hotuba yake kwenye Baraza hilo la Idd
 Kinamama kwenye Baraza hilo la Eid ElFitr
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa na Mama Shamim Khan kwenye Baraza hilo la Eid 
 Mwanazuoni akighani kaswida maalum kwenye Baraza hilo la Idd
Wanazuoni wakitumbuiza kaswida kwenye Baraza la Idd
 Ustaadhi Mroki Mroki wa Habari leo akifuatilia kwa makini shughuli za hafla hiyo ya Baraza la Eid
 Baadhi ya Wasanii maafurufu wa Bongo Movie akiwemo Steve Nyerere  nao walihudhuria Baraza hilo
Membe akiagana na wadau baada ya shughuli za Maulid. Picha zote na Bashir Nkoromo- theNkoromo Blog

No comments: