Tangazo

October 19, 2012

WAISLAMU MARUFUKU KUANDAMANA DAR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki
 DAR ES SALAAM

Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam wamekutana na kutoa tamko la kuzuia waislamu kuacha kuandamana mara moja.

Katika taarifa ya waliyoitoa mapema leo asubuhi wakuu na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo wa dini wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadick, (picha ya chini) aliwatoa hofu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani wamejipanga kulinda hali ya amani.

Akitoa tamko hilo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa kumekuwapo na taarifa za waumini wa Kiislamu kuandamana na kufanya fujo mara baada ya swala ya Ijumaa na baadala yake amewataka kuacha kufanya hivyo na warejee majumbani kwa amani na suala hilo linashughulikiwa kisheria.

Hata hivyo kwa upande wao viongozi wa dini waliokutana na Mkuu wa mkoa  juu ya kutolea tamko hilo waliwaasa waumini wote kutoingia mitaani na kuandamana kwani wakifanya hivyo ni kukiuka misingi mbalimbali  ya kisheria iliyopo kihalali na watakapofanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi.

Kamanda Kova
Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Musa bin Salum amewataka wakuu wa misikiti mkoa wa Dar es Salaam kuwakataza waumini hao kufanya maandamano kwani kufanya hivyo ni kukiuka misingi iliyopo.Aidha, aliwaomba waumini warejee majumbani  kwa amani.

Askofu  Makunda aliwataka watanzania kuendelea kufuata misingi ya kiimani bila chuki wala kufanya fujo.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova (pichani juu) alitoa onyo kali kwa waislamu kuacha kufanya hivyo hii leo kwani kwa atakaekiuka atachukuliwa hatua kali. Kova aliwataka waumini kurejea majumbani mwao kwa amani bila kufanya maandamano  na pia aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kupuuza tishio hilo la fujo kutoka kwa waislamu.

“Jeshi limejipanga kuakikisha hali ya amani na usalama inakuwepo hivyo taadhari kwa waislamu kuacha kufanya maandamano mara moja” alisema Kova kwenye kikao hicho ambacho kinaendelea hivi sasa.

Wakuu hao wamekutana kwa dharura baada ya kuwepo kwa taarifa za juu ya waumini hao kutishia kuandamana  na kufanya fujo.

No comments: