Tangazo

Tangazo

Tangazo

Tangazo

Tangazo

Tangazo

November 22, 2014

Rais Kikwete atolewa nyuzi katika mshono na Afya yake yazidi kuimarika

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita.Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri. Kulia kwake ni Daktari wa Rais Prof. Mohamed Janabi
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepumzika kwenye hoteli maalumu baada ya kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland alikotolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume wiki iliyopita..Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri. Picha na Freddy Maro

Mwanahabari Mwandamizi wa New Habari 2006 Ltd, Marehemu Munyuku aagwa jijini Dar

Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
 Mwandishi wa habari wa gazeti la Hoja, Iche Mang'enya akitoa heshima za mwisho.
 Mhariri Mtendaji Mkuu wa New habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda akitoa heshima za mwisho. Kushoto Mwandishi wa habari wa gazeti la Hoja, Iche Mang'enya akitoa heshima za mwisho.
 Matinyi akisoma wasifu wa marehemu.
 Mwakilishi wa klabu ya Yanga, Said Motisha akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya klabu yake ambapo alitoa ubani wa sh. laki tano.
 Motisha akikabidhi ubani wa sh. laki tano.
 Mmoja wa watu waliosoma na marehemu Munyuku akitia salama za rambirambi ambapo walitoa sh. laki tatu.
  Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando akitoa salama za rambirambi.
 Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda akitoa salam za rambirambi.
 Mwakilishi wa familia, Mkuchika akitoa neno la shukrani.
 Rashid Kejo akitoa salama za rambirambi.
 Mwakilishi wa Uhuru Publishers akitoa salama za rambirambi na ubani wa sh. laki mbili.
 Waombolezaji wakielekea katika gari kwa ajili ya safari ya Morogoro kwa mazishi ya marehemu Inocent Munyuku.
 Mwili wa marehemu Munyuku ukiingizwa katika gari tayari kwa safari ya kwenda mkoani Morogoro kwa mazishi.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd wakiwa katika hospitali ya Lugalo wakati wa kuaga mwili wa marehemu Inocent Munyuku.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika hospitali ya Lugalo wakati wa kuaga mwili wa Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, marehemu Inocent Munyuku.
 Mwandishi wa gazeti la Jamhuri, Alfred Lucas (kushoto) na Limonga Justine Limonga wa Radio Uhuru.
 Waombolezaji.
 Msanifu Mkuu wa Kurasa wa gazeti la Tanzania Daima, Emily Maya akimpa pole Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda.
Mkurugenzi wa Global Publisher, Eric Shigongo akiteta jambo na Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda.

DORIS MOLLEL ACHANGIA VITABU SHULE YA MSINGI MPUNGUZI, DODOMA KWA USHIRIKIANO NA MAK SOLUTIONS LTD

1
Doris Mollel akikabidhiwa vitabu 200 na mkurugenzi wa MAK Solutions Bi Meetal Kirubakaran. Vitabu hivyo vilikabidhiwa kwa shule ya msingi Mpunguzi iliyopo Dodoma kama mchango wa kuadhimisha siku ya watoto duniani.(Picha zote na Albert Manifester).

Dodoma, Novemba 2014.

Katika kuadhimisha siku ya watoto duniani inayofanyika tarehe 20 Novemba kila mwaka, Mrembo wa Redds Miss central Zone 2014 Doris Mollel amechangia Vitabu vyenye thamani ya Shilingi Milioni moja (1,000,000/=) katika shule ya msingi Mpunguzi iliyopo katika kijiji cha Mpunguzi mkoani Dodoma.

Doris, ambaye pia ni mshindi wa tatu kwenye Redds Miss Tanzania 2014 amejikita katika sekta ya elimu kama sehemu ya huduma zake za jamii ambapo amedhamiria kuendeleza mchango kwenye elimu ya msingi kwa kuchangia vitabu kwenye shule zenye uhitaji zaidi.

Msaada huo wa Vitabu 200 vya kiada na ziada ameutoa kwa ushirikiano na kampuni ya uuzaji wa Vitabu ya MAK Solutions yenye duka lake Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bi Meetal Kirubakaran alisema MAK solutions wanafurahi kutoa vitabu hivyo kama mchango wao katika kusaidia sekta ya elimu Tanzania.
2
Doris akijadiliana jambo na Afisa elimu wa mkoa wa Dodoma Bw. Juma Kaponda (Katikati) mjini Dodoma kabla ya kuelekea Mpunguzi. Wa kwanza kushoto ni Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo na anayefuata ni Afisa elimu – Taaluma wa mkoa Bw Eliud Njogela.

Akizungumza kwenye hafla iliyofanyika shuleni hapo, Mollel alisema ‘Ni muhimu kuwajengea watoto wetu utamaduni wa kujisomea tangu wakiwa wadogo ili kuwakuza kukabiliana na changamoto za dunia ya sasa ambayo inahitaji uelewa mpana. Najivunia kuwa sehemu ya kampeni hii na nitaendelea kuongeza jitihada za kuwafikia watoto wengi zaidi’

Afisa elimu wa mkoa wa Dodoma Bw. Juma Kaponda amempongeza Doris kwa juhudi zake za kusadia jamii hasa sekta ya elimu na ameomba wadau wengi kuiga mfano huu kuendeleza sekta hii.

Hafla hiyo ya makabidhiano ilihuduriwa na mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mpunguzi Bi Neema Mando, Makamu mwalimu mkuu wa shule Bw Danctan Chipalo, Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo, Afisa elimu – Taaluma wa mkoa Bw Eliud Njogela pamoja na wanafunzi wote wa shule ya Mpunguzi.
3
Alipokuwa njiani kuelekea mpunguzi, Doris alipata nafasi ya kuongea machache na baadhi ya wanafunzi wa vijiji vya jirani.
4
Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini.
5
Doris Mollel (kulia) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili shuleni Mpunguzi. Kushoto ni Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo na katikati ni mwalimu mkuu wa shule ya mpunguzi Bi Neema Mando.
6
Doris akiuleza uongozi wa shule nia na madhumi ya safari yake. Kushoto ni mwalimu mkuu msaidizi Bw Danctan Chipalo na mwalimu mkuu Bi Neema mando.
7
Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo akimsaidia Doris kuchambua vitabu hivyo kutoka kwenye boksi la MAK Solutions Ltd.
8
Doris akiwaeleza wanafunzi umuhimu wa kupenda kujisomea tangu wakiwa wadogo.
9
Kutoka kushoto: Bw Danctan Chipalo, Bw Mnyagatwa Mazengo Bi Neema Mando na Doris.
10
Doris akiwa na baadhi ya wanafunzi baada ya kugawa vitabu.
11
Wanafunzi wakifurahia vitabu vyao.
12
Akimuelekeza mmoja wa wafunzi juu ya mambo yaliyomo kwenye kitabu cha ‘WATER’
13
Wakiwa na Vitabu.
14
Makabidhiano.
15
Doris akiongea jambo na mwalimu mkuu mara baada ya makabidhiano hayo.
16
Akiwa kwenye picha ya pamoja kwenye viwanja vya shule hiyo muda mfupi kabla ya kuondoka shuleni hapo.

KAMPUNI YA PAN AFRICAN ENERGY YATOA MSAADA WA MIFUKO 1500 YA SARUJI KWA WILAYA YA KILWA

Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za Jamii wa Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya Pan African Energy, Andrew Kashangaki (kwanza kushoto) akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Peter Malekela (kulia) msaada wa saruji 1,500 yenye thamani ya shilingi milioni 18 kwa halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Lindi ili kuwezesha ujenzi wa maabala 59 katika shule zake za sekondari zipatazo 24. Pembeni wanaoshuhudia ni viongozi wa halmashauri hiyo na wafanyakazi wa Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya Pan African Energy. Makabidhiano hayo yalifanyika mwanzoni mwa wiki Novemba 17, 2014 katika kiwanda cha Saruji cha Kilwa, Lindi. (Picha zote na Cathbert Kajuna.)
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya Peter Amosi Malekela akizungumza machache.
Waandishi wa habari wakifanya mahojiano na mwalimu wa masomo ya sayansi wa shule ya sekondari Mtanda ambapo uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa na viongozi toka kampuni ya  Pan African Energy (T) Ltd.
Moja ya Maabala inayojengwa kwa msaada wa Pan African Energy (T) Ltd.
Moja ya mradi wa Nyumba ya Madaktari inayojengwa kwa msaada wa kampuni hiyo.
Moja ya Hospitalli ya Nangurukuru ikiwa imekwosha tayari kwa
Mazungumzo ya hapa na pale.
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Peter Malekela (kulia) akiongea na wageni wake waliomtembelea ofisini kwake.
Msafara ukielekea eneo la tukio.
Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa na viongozi toka kampuni ya  Pan African Energy (T) Ltd wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya Pan African Energy imetoa msaada wa mifuko 1500 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 18 kwa halmashauri ya wilaya ya Kilwa ili kuwezesha ujenzi wa maabala katika shule zake za sekondari.
Akikabidhi msaada huo Andrew Kashangaki, Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za Jamii wa kampuni hiyo alisema wao wametoa msaada huo ili kuweza kutimiza lile agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuzitaka kila shule za sekondari kuwa na maabala ifikapo Novemba 30, 2014.
“Kampuni yetu imewekeza huku hivyo ni vyema kuendeleza eneo ambalo limewekeza ikiwa ni kutoa huduma kwa jamii inayotuzunguka likiwemo suala la elimu bora na afya kwa ujumla ndiyo maana umeona leo tumekabidhi msaada wa mifuko hii ya saruji,” alisema Bw. Kashangaki.
Bw. Kashangaki alisema kampuni yao, mbali na Aliongeza kuwa mbali na utoaji wa msaada huo, kampuni ya Pan African Energy alishajenga hospitali katika eneo la Nangurukuru ambao imekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa huko.
Pia alishukuru halmashauri ya Wilaya hiyo kwa uaminifu iliyouonyesha kwa kuanza kutumia saruji hizo kama zilivyokusudiwa.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa, Peter Malekela aliishukuru kampuni hiyo kwa kile walichotoa ambacho kwa kiasi kikubwa kimesaidia kuleta maendeleo katika wilaya yao jambo linaloleta faraja kwa wananchi.
Bw. Malekela alisema saruji waliyoipata waliigawanya kwa shule 24 za wilaya hiyo ambazo jumla ya maabala 59 zinahitaji, ambapo shule ya Kikanda, Kandawale, Miguruwe, Kiranjeranje, Nakiu, Likawale, Kikole, Pande, Mtanga, Njinjo, Namayuni, Kibata hizi zote zinahitaji maabala tatu (3) na mgao wa mifuko 76 ya saruji kila moja.
Nyingine ni shule ya sekondari Miteja, Mpunyule, Matanda, Songosongo, Dodomezi, Kivinje, Mibuyuni, Kipatimu, Alli Mchumo, Migumbi, Kijumbi hizi nazo zinahitaji maabala 2 kila moja na zinapata mgao wa mifuko 51 kila moja. Shule ya mwisho ni Kila yenyewe inahitaji maabala moja na imepata mgawo wa mifuko 25 ya saruji.
“Kila tunapopita tumekuwa mabalozi wenu wazuri kusema yale mazuri ambao mmekuwa mkiyafanya kwa wilaya yetu, tokea kampuni hii imeingia maendeleo ya eneo hili yanaonekana tofauti na zamani. Tunawaomba muendelee na moyo huu wa kujitolea na tunaalika makampuni mengine yaje tuijenge Kilwa yetu,” Alisema Bw. Malekela.